Kwa mujibu wa ketengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Maulana Hidayat-ur-Rahman Baluch, Amir wa Jamaa'tul Islamia ya Baluchistan na mwanachama wa bunge la mkoa, katika hafla iliyofanyika kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Imam Khomeini (ra) mjini Quetta, Pakistan, alitaja nafasi yake kuu katika kuamsha mataifa na kuunga mkono wanyonge duniani, akasema: Jina la Imam Khomeini (ra) linawakumbusha kila mara uvumilivu, ulinzi wa haki za wanyonge na mshikamano wa Kiislamu.
Aliongeza kwa kusisitiza kwamba Imam Khomeini (ra) hakuliamsha tu taifa la Iran, bali pia alikuwa ni sauti iliyo wazi kwa wanyonge wote duniani, hasa taifa lililo dhulumiwa la Palestina, kisha akasema: Imam Khomeini (ra) kutokana mapinduzi yake ya kihistoria na kusimamisha Mageuzi ya Kiislamu, aliyafungulia mataifa njia mpya na kuamsha dhamira zilizo macho. Leo hii ujumbe wa huyo mtu mkuu wa historia bado unatoa msukumo kwa walingania uhuru na wapiganaji wa haki duniani kote.
Maulana Hidayat-ur-Rahman alibainisha kuwa: Kulinda haki za mataifa na kupigana dhidi ya dhulma na ukandamizaji ni jukumu la kidini, la maadili na la kibinadamu. Katika hali ya sasa ambapo watu wa Palestina, hasa Ghaza, wakiwa wanamiminiwa mabomu na huku wamezingirwa kikatili na utawala wa Kizayuni, si Marekani na Israeli pekee wanaowajibika kwa hayo mauaji, bali pia baadhi ya wafalme na viongozi wa nchi za Kiislamu kwa sababu ya ukimya wao na kupuuza, pia ni washirika wa dhuluma hiyo.
Maoni yako